Ni lazima kwa mwanaume anayefiliwa na mkewe kusubiri masiku kadhaa kabla ya kuoa mke mwengine?

Swali: Pindi mwanamume anapofiliwa na mke wake na akataka kumuoa dada wa huyo mwanamke ni lazima kwake kusubiri kiasi masiku ya eda ya yule mwanamke? Naomba kupewa fatwa katika mambo haya. Je, katika hali hii mwanaume anakaa eda?

Jibu: Sio lazima kwa yule anayefiliwa na mke wake na akataka kumuoa dada wa huyo mwanamke kusubiri kiwango cha eda yake kwa sababu ya kutokuwepo haja ya kufanya hivo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (18/11)
  • Imechapishwa: 04/08/2017