Ni lazima kwa mwanamke kufunika miguu yake


Swali: Inajuzu kwa mwanamke kurefusha vazi lake chini ya nyoyo zake takriban sentimeta tano?

Jibu: Ndio, inafaa kwa mwanamke kuiteremsha nguo yake chini ya kongo zake za miguu. Bali jambo hili ndilo limewekwa katika Shari´ah juu yake ili aweze kuifunika miguu yake. Kufunika miguu ya mwanamke ni jambo lililowekwa katika Shari´ah. Bali ni jambo la lazima kwa mujibu wa wanachuoni wengi. Linalompasa mwanamke ni yeye kuifunika miguu yake. Anaweza kufanya hivo ima kwa nguo inayoteremka juu yake au kwa kuvaa soksi, viatu au mfano wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (16) http://binothaimeen.net/content/6806
  • Imechapishwa: 11/03/2021