Ni lazima kwa msafiri kuswali msikitini

Swali: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa msafiri kuswali pamoja na mkusanyiko msikitini?

Jibu: Ndio. Ikiwa anasikia adhaana na anaishi karibu na msikiti, basi haijuzu kwake kuswali nyumbani kwake. Bali anatakiwa kwenda kuswali pamoja na mkusanyiko:

“Mwenye kusikia adhaana na asiiendee, basi hana swalah isipokuwa akiwa na udhuru.” Wakasema: “Ni udhuru upi, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Khofu au maradhi.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (92) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/%D8%A5%D8%BA%D8%A7%D8%AB%D8%A9%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%D9%81%D8%A7%D9%86%20%D9%85%D9%86%20%D9%85%D8%B5%D8%A7%D8%A6%D8%AF%20%D8%A7%D9%84%D8%B4%D9%8A%D8%B7%D8%A7%D9%86-29-07-1439%D9%87%D9%80%200010.mp3
  • Imechapishwa: 22/07/2018