Ni lazima kwa mke pia kutoa kafara midhali alifanya kwa raha zake


Swali: Kuna mwanamume alimwingilia mke wake mchana wa Ramadhaan ambapo akafunga miezi miwili mfululizo. Je, kuna kinachomlazimu mke wake?

Jibu: Analazimika kufanya mfano wake ikiwa alifanya kwa kutaka kwake mwenyewe na hakulazimishwa. Akishindwa basi awalishe masikini sitini. Kiwango chake ni karibu 1,5 kg ya chakula. Ama ikiwa alimlazimisha kwa nguvu na kwa kumpiga sana basi hakuna kinachomlazimu. Katika hali hiyo dhambi zitamwendea mume tu. Lakini ikwa alimchukulia wepesi basi na yeye ni lazima atoe kafara kama mfano wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/302)
  • Imechapishwa: 01/06/2018