Ni lazima kwa mayahudi na manaswara kuingia katika Uislamu?

Swali: Je, mayahudi na manaswara baada ya kutumwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni lazima kuingia katika Uislamu?

Jibu: Hapana shaka. Ni lazima kwa viumbe wote, watu na wanaadamu, kuingia katika Uislamu na kumfuata  Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yule asiyemfuata ni kafiri. Ni mamoja akawa mayahudi, mnaswara au mwengine. Asiyemfuata ni kafiri ambaye amemkana Allaah (´Azza wa Jall). Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hatosikia yeyote kuhusu mimi, myahudi au mnaswara, halafu asiamini yale niliyokuja nayo isipokuwa ataingia Motoni.”

  • Mhusika: Imaam Swalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=oMoaMLGx4k0
  • Imechapishwa: 19/11/2017