Ni lazima kwa daktari kuficha siri za mgonjwa

Swali: Hujiwa na wagonjwa ambao wamepewa mtihani wa kutumia ulevi na mada ya kulevya. Matokeo yake yanawapekea kufanya baadhi ya uhalifu kama mfano ya uzinzi na liwati. Je, nikawaripoti?

Jibu: Ni lazima kwako kuwanasihi. Unatakiwa kuwanasihi, kuwahimiza watubu, kuwasitiri, usiwashtaki, usiwafedhehi na uwasaidie juu ya kumtii Allaah na Mtume Wake. Waeleze kwamba Allaah anamsamehe mwenye kutubia. Watahadharishe kurudi katika maasi haya. Allaah (Subhaanah) amesema:

وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ

“Waumini wanaume na waumini wanawake ni marafiki wao kwa wao; wanaamrisha mema na wanakataza maovu.”[1]

وَالْعَصْرِ إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ

“Naapa kwa al-‘Aswr. Hakika ya mwanaadamu bila ya shaka yumo katika khasara. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema na wakausiana kwa kufuata ya haki na wakausiana kuwa na subira.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Dini ni kupeana nasaha… “

“Mwenye kumstiri muislamu basi Allaah atamsitiri duniani na Aakhirah.”

Mbili hizo zimepokelewa na Imaam Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

[1] 09:71

[2] 103:01-03

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/436)
  • Imechapishwa: 31/07/2021