Ni lazima kwa baba kuwahijisha watoto wake waliobaleghe?

Swali: Kuna mtu ana watoto wa kiume na wa kike ambao tayari wamekwishabaleghe. Lakini hawana uwezo wa kimali. Je, ni lazima kwa baba yao kuwatolea pesa kiasi kitachowawezesha kufanya hajj au wasubiri mpaka pale watapokuwa na uwezo wao wenyewe?

Jibu: Sio lazima kwa baba kuwahijisha watoto wake hata kama atakuwa na mali nyingi. Hii ni dini. Ikipatikana kwao sharti, ambayo ni kule kuwa na uwezo wao wenyewe, hapo itakuwa ni wajibu kwao. Lakini wakumuomba baba yao na akawawahijisha ni jambo zuri. Hapana shaka kwamba baba huyu anapata thawabu. Lakini, je, ni wajibu kwake kuwawahijisha? Hapana, si wajibu kwake. Pengine tukasema kwamba ni wajibu ikiwa kama amehijisha baadhi yao na akaacha wengine. Katika hali hii tunasema kuwa ni lazima kuwahijisha wale wengine kwa kujengea uwajibu wa kufanya uadilifu. Wale wengine wakitoa idhini na wakamwambia baba yao kwamba yeye ndiye ana khiyari ya kuwahijisha au kutowahijisha, basi baba huyo anakuwa si mwenye kulazimika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (53) http://binothaimeen.net/content/1187