Ni lazima kwa anayepata hedhi na nifasi mchana wa Ramadhaan kujizuia?

Swali: Ni lazima kwa mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi kujizuia na kula na kunywa wakisafika mchana wa Ramadhaan?

Jibu: Mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi wakisafika mchana wa Ramadhaan sio wajibu kwao kujizuia na kula na kunywa. Anapata ruhusa ya kula na kunywa. Kujizuia kwake hakuna maana yoyote kwa kuwa ni wajibu kwao kuilipa siku hiyo. Haya ndio maoni ya Maalik, ash-Shaafi´iy na Imaam Ahmad. Imepokelewa vilevile kutoka kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba amesema:

“Mwenye kula mwanzoni mwa mchana basi na ale mwishoni mwake.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/99)
  • Imechapishwa: 03/06/2017