Ni lazima kuwaamrisha watoto kufunga wanapofikisha miaka saba

Swali: Mvulana ambaye ana uwezo wa kupambanua aamrishwe kufunga? Swawm hiyo itakuwa ni sahihi kwake iwapo atabalaghe katikati ya funga?

Jibu: Watoto wa kiume na wa kike wanapofikisha miaka saba wanatakiwa kuamrishwa kufunga ili waweze kuzowea. Ni lazima kwa walezi wao kuwaamrisha kufanya hivo kama ambavo wanawaamrisha swalah. Watapobaleghe basi ni lazima kwao kufunga. Wakibaleghe katikati ya mchana basi hiyo itakuwa itakuwa ni sahihi kwao. Iwapo tutakadiria kuwa mtoto wa kiume amekamilisha miaka kumi na tano kabla ya jua kuzama ilihali amefunga, basi siku hiyo itahesabika kwake. Mwanzoni mwa mchana huo itakuwa swawm yake ni sunnah na mwishoni mwake itakuwa ni faradhi. Ikiwa alikuwa hajabaleghe kabla ya hapo, kwa kuota nywele sehemu za siri au kumwaga manii kwa matamanio – hukumu hii inamuhusu vilevile mtoto wa kike isipokuwa tu msichana kuna jambo la nne linalozidi kwake ambapo anaweza kubaleghe kwa kupata hedhi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/180-181)
  • Imechapishwa: 16/05/2018