Ni lazima kuwa na wudhuu´ wakati wa kumswalia maiti?

Swali: Imeshurutishwa kwa mswaliji awe na wudhuu´ wakati wa kumswalia maiti?

Jibu: Ndio, ni swalah. Swalah haisihi isipokuwa mtu awe na wudhuu´. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ

”Enyi walioamini!  Mnaposimama kwa ajili ya swalah, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi na futeni vichwa vyenu na [osheni] miguu yenu hadi kwenye vifundo.” (05:06)

Hili n ijambo lenye kuenea. Linahusu swalah ya jeneza, swalah za faradhi, swalah za Sunnah, swalah ya kupatwa kwa jua na swalah ya idi. Inahusu swalah zote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (67) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah22-05-1438h.mp3
  • Imechapishwa: 18/10/2017