Ni lazima kumuamsha mtoto chini ya miaka saba kuswali Fajr?

Swali: Mimi nina mvulana aliye na miaka nane. Je, nimuamshe katika swalah ya Fajr? Nisipofanya hivo napata dhambi?

Jibu: Dhahiri ni kwamba hili linatakiwa kuangaliwa; ikiwa ni wakati wa majira ya baridi na na wakati mgumu hakuna neno kumuacha na pindi atapoamka anatakiwa kuambiwa aswali.

Ama ikiwa hali ya hewa ni ya kawaida na haina madhara juu yake, basi anatakiwa kuamshwa ili azowee kuswali pamoja na wengine. Leo, na himdi zote anastahiki Allaah, kuna watoto walio kati ya miaka saba mpaka kumi tunawaona wanakuja pamoja na baba zao katika swalah ya Fajr. Mtoto akizowea hilo tokea mdogo basi ndani yake kunakuwa kheri nyingi. Ama ikiwa kuna uzito si wajibu kwako kumuamsha. Lakini hata hivyo unatakiwa kumuamrisha kuswali pale atapoamka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (40) http://binothaimeen.net/content/911
  • Imechapishwa: 16/09/2018