Ni lazima kumsaidia mume wangu katika kutaka kuongeza mke mwingine?


Swali: Je, ni wajibu kwa mke kumtii mume wake katika kuoa juu yake mke wa pili pamoja na kujua ya kwamba anashurutisha awe ni mwenye umri mdogo na mzuri na mke wa kwanza ndio amsimamie katika kumuoea?

Jibu: Anayoweza mume kumuomba mke wake ni mambo aina mbili:

1- Mambo ambayo Allaah kamuwajibishia mke. Miongoni mwa mambo hayo ni kushughulikia kazi za nyumbani, kumsaidia kumtazamia na kumlelea watoto, kufanya nae jimaa, kujisitiri wakati mume hayupo na kusaidia katika mambo ambayo yatatengeneza hali zao katika uwepo wa mume.

2- Mambo ambayo sio lazima juu yake mke. Miongoni mwa hayo, ni yalokuja katika swali hili. Sio lazima kwake mke kutii jambo lake wakati anapotaka kuoa mwanamke mwingine. Akijitolea na akafanya hivyo, hakuna neno. Akikataa, si juu ya mume kumlazimisha mke kwalo.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/2978
  • Imechapishwa: 20/09/2020