Ni lazima kumraddi mzushi anayelingania katika Bid´ah

Swali: Kuhusiana na kurudiana, baadhi ya watu wamesema kuwa asiraddiwe kila mmoja na wakasema:

“Ni nani atakayebaki endapo ataraddiwa kila mmoja?”

Je, haya ni sahihi?

Jibu: Hapana, haya sio makusudio. Watu hawatakiwi kukemeana katika mambo ya Ijtihaad. Kwa mfano mmoja anaonelea kuwa nyama ya ngamia inachengua wudhuu´ na mwengine haonelei hivo. Katika halii huyu wa kwanza hatakiwi kumraddi huyu wa pili.

Kuhusu mzushi anayelingania katika Bid´ah, ni lazima araddiwe. Bid´ah sio suala la ki-Ijtihaad. Salaf wote wameafikiana juu ya kutupilia mbali Bid´ah. Hapa hakuna jambo la kufadhilishana.

Kuhusu mambo ya ki-Fiqh yaliyojengeka juu ya Ijtihaad na ambayo wanazuoni wametofautiana, haitakiwi kumraddi kila yule anayekwenda kinyume na maoni ya mwengine. Endapo tutafungua mlango huu, basi kila mmoja angelikuwa mwenye kumraddi mwenzie.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (127 B) Tarehe: 1417-01-27/1996-06-13
  • Imechapishwa: 12/07/2021