Ni lazima kumpa mtoto jina ile siku ya saba?

Swali: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kumpa mtoto jina siku ile ya kwanza anapozaliwa au ni lazima iwe katika siku ya saba pamoja na kufanyiwa ´Aqiyqah?

Jibu: Sio lazima iwe siku ya saba. Anaweza kumwita siku yoyote anayopenda. Hakuna neno. Anapozaliwa, baada ya kuzaliwa, siku ya saba na kadhalika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-28-1-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 06/10/2020