Swali: Mmoja katika jamaa zangu haswali na ni mtumzima. Nimemnasihi na akanasihiwa na watu wengi lakini hata hivyo anapuuza sana swalah isipokuwa mara chache. Wakati mwingine haswali isipokuwa katika Ramadhaan au ijumaa peke yake. Natakiwa kuchukua msimamo gani juu yake? Je, nimtolee salamu nikimkuta kwenye kikao au nimsuse?

Jibu: Kuacha swalah kwa makusudi ni ukafiri mkubwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Baina ya mtu na shirki na ukafiri ni kuacha swalah.”

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Amesema tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

 “Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao [makafiri] ni swalah. Hivyo basi, yule mwenye kuiacha amekufuru.”

Amepokea Imaam Ahmad na watunzi wa as-Sunan kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Zipo Hadiyth nyingi zenye maana kama hiyo.

Kwa hivyo ni lazima kumnasihi mlengwa na kumbainishia hukumu ya Shari´ah. Akiendelea kuacha swalah basi italazimika kumkata, kuacha kumtolea salamu, kutomwitikia mwaliko wake na kumshtaki kwa mtawala ili amwambie kutubia. Akitubia ni vyema na vyenginevyo ni lazima kumuua. Amesema (Ta´ala):

فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ

“Lakini wakitubu na wakasimamisha swalah na wakatoa zakaah, basi waacheni huru.”[1]

Ikafahamisha kwamba asiyesimamisha swalah basi haachwi huru. Zipo dalili nyingi juu ya jambo hilo.

[1] 09:05

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/268)
  • Imechapishwa: 11/09/2021