Ni lazima kujisafisha kwa maji kwa ambaye alijisafisha kwa mawe?

Swali: Mtu akiosha sehemu zake za siri baada ya kupatwa na hadathi na ukafika wakati wa swalah – je, aoshe sehemu zake za siri upya wakati wa kutaka kutawadha?

Jibu: Hapana. Mtu akijisafisha kwa mawe au kitu mfano wake wakati amekojoa kisha ukafika wakati wa swalah hana haja ya kurudi kujisafisha mara nyingine. Kwa sababu kujisafisha kwa mawe ni kuondosha najisi. Najisi ikiondoka kuna haja yoyote ya kurudi kujisafisha kwa maji wakati wa kutawadha? Hapana. Kwa ajili hii Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ

“Mkiwa na janaba, basi jitwaharisheni na mkiwa wagonjwa au mko safarini au mmoja wenu akija kutoka msalani au mmewagusa wanawake kisha hamkupata maji, basi fanyeni Tayammum kwa ardhi kwa juu panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu.”[1]

Hakutaja kujisafisha kwa mawe au kitu mfano wake. Kwa sababu kujisafisha kwa mawe ni kuondosha najisi. Pindi utapoiondosha wakati wowote basi inaondoka na hapana haja ya kurudi kujisafisha mara nyingine kwa maji.

[1] 05:06

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (54) http://binothaimeen.net/content/1219
  • Imechapishwa: 08/07/2020