Ni lazima kufunga siku sita za Shawwaal kwa kufululiza?


Swali: Je, ni lazima kwa mwenye kufunga siku sita za Shawwaal kufululiza au hakuna ubaya kufunga kwa kuachanisha siku midhali ni ndani ya mwezi?

Jibu: Kufunga siku sita za Shawwaal ni Sunnah iliyothibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Inafaa kufunga kwa kufululiza au kwa kuachanisha siku. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kufunga kwa kuachia na hakutaja jambo la kufululiza wala kuachanisha masiku. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atakayefunga Ramadhaan kisha akaifuatishia siku sita za Shawwaal basi ni kama ambaye amefunga mwaka mzima.”[1]

Ameipokea Imaam Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

[1] Muslim (1164), at-Tirmidhiy (759), Abu Daawuud (2433), Ibn Maajah (1716), Ahmad (05/417) na ad-Daarimiy (1754).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/391)
  • Imechapishwa: 09/06/2018