Ni lazima alipe deni la watu

Swali: Kuna mtu alikopa 100.000 SAR kutoka benki na atalipa deni hilo kwa ribaa ya 20% ambapo baadaye atalipa 120.000 SAR. Ni ipi hukumu ya mkopo huu?

Jibu: Ni kwa nini anauliza baada ya kuwa amekwishakopa. Je, anataka kukwepa kulipa? Si sawa kufanya hivo. Anatakiwa kulipa deni, apate dhambi na ahakikishe harudi tena kufanya kitendo kama hicho.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (19) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdtfq-22011435-01.mp3
  • Imechapishwa: 20/12/2019