Swali: Baadhi ya waandishi wa leo wametaja kwamba mwenye kusema au kutenda kitu cha kufuru hakufuru mpaka asimamishiwe hoja na wamewapitisha waabudu makaburi katika njia hiyo.

Jibu: Haya ni kutokana na ujinga wao. Waabudu makaburi ni makafiri. Mayahudi ni makafiri. Manaswara ni makafiri. Lakini wakati wa kuwaua wanatakiwa kuambiwa watubie na la sivyo wauwawe.

Swali: Lakini masula ya kusimamisha hoja. Je, ni lazima kuwasimamishia hoja?

Jibu: Wamefikiwa na Qur-aan:

هَـٰذَا بَلَاغٌ لِّلنَّاسِ

“Huu ni ufikisho wa ujumbe kwa watu.”[1]

Imewabainikia kati ya waislamu:

وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ

”Nimefunuliwa hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itayomfikia.”[2]

هَـٰذَا بَلَاغٌ لِّلنَّاسِ

“Huu ni ufikisho wa ujumbe kwa watu.”[3]

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ

“Ee Mtume! Fikisha… ”[4]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewafikishia, Qur-aan imewafikia na iko kati yao na wanaisikia kwenye idhaa na kwenginepo. Lakini wanapuuza. Anapokuja mtu kuwakataza wanamfanyia uadui.

[1] 14:52

[2] 06:19

[3] 14:52

[4] 05:67

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-is-Shubuhaat, uk. 141-115
  • Imechapishwa: 21/08/2019