Ni kweli Ibn Baaz amejuzisha kuswali Dhuhaa´ bila wudhuu’?

Swali: Nimemsikia mtu akimnukuu ´Allaamah Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) kwamba ametoa fatwa kujuzu kufaa kuswali swalah ya Dhuhaa’ pasi na wudhuu´?

Jibu: Maneno haya ni batili. Ni maafa yepi ya khabari isipokuwa wapokezi wake pale walipomkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)! Maneno haya si kweli. Swalah haisihi pasi na wudhuu´ kwa maafikiano ya waislamu. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ

“Enyi walioamini! Msikaribie swalah na hali mmelewa mpaka mjuekile mnachokisema na wala mkiwa mna janaba isipokuwa mmo safarini mpaka muoge josho na mkiwa wagonjwa au safarini au mmoja wenu ametoka msalani au mmewagusa [kuwajamii] wanawake kisha hamkupata maji, basi fanye Tayammum kwa ardhi safi ya mchanga – pakeni nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kusamehe.”[1]

[1] 04:43

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (10) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191426#219753
  • Imechapishwa: 10/05/2019