Swali: Tumesikia Shaykh al-Luhaydaan akimtetea Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy na kusema kuwa ni katika wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah. Baada ya hapo baadhi wakaanza kueneza tuhumu za kwamba wewe unamfanyia Tabdiy´ Shaykh Rabiy´ na kumtoa katika mzunguko wa Sunnah…[1]

ar-Raajihiy: Ni nani alosema haya? Ni nani alosema haya? Ni nani alosema haya?

Muulizaji: Yapo kwenye Intaneti.

ar-Raajihiy: Ni nani aliyenukuu haya kutoka kwangu? Muulizaji: Yapo kwenye Intaneti. Kuna Haddaadiyyah wanaoyaeneza.

ar-Raajihiy: Kila kinachoenezwa ni kweli?

Muulizaji: Nini?

ar-Raajihiy: Kila kinachoenezwa ni kweli? Muulizaji: Hapana.

ar-Raajihiy: Kila kinachoenezwa ni kweli?

Muulizaji: Hapana.

ar-Raajihiy: Walimsemea uongo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Muulizaji: Shaykh Rabiy´ ni katika wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah?

ar-Raajihiy: Wakati walipokuja kwa Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) na kumtuhumu ya kuwa amesema haya na yale juu yao, akasema: “Wamenisemea uongo.” Walimsemea uongo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)… Ni uongo.

Muulizaji: Ninukuu kutoka kwako ya kwamba Shaykh Rabiy´ ni katika wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah?

ar-Raajihiy: Nukuu kutoka kwangu, nukuu kutoka kwangu… [sauti haiko wazi]

Tazama http://www.wanachuoni.com/content/wanafunzi-wanaomsema-vibaya-al-fawzaan-al-%C2%B4abbaad-na-al-madkhaliy

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=146670
  • Imechapishwa: 08/05/2018