Ni kwanini ufahamu wa Salaf?


Swali: Ni kwa nini wanachuoni siku zote wameambatanisha mtu kufuata Qur-aan na Sunnah kwa ufahamu wa Salaf-us-Swaalih…

Jibu: Kwa sababu wao ndio walikuwa karibu na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wamesalimika na tofauti iliotokea baada yao. Wao ndio wako karibu zaidi na haki kuliko wengine. Maswahabah walichukua elimu kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Taabi´uun walichukua elimu kutoka kwa Maswahabah. Waliokuja baada ya Taabi´uun walichukua elimu kutoka kwa wale waliochukua elimu kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wao ndio waaminifu zaidi kwa ushahidi wa Aayah:

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ

“Wale waliotangulia awali miongoni mwa Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema, Allaah ameridhika nao nao wameridhika Naye na amewaandalia mabustani yapitayo chini yake mito – ni wenye kudumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.” (09:100)

Ni jambo liko wazi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (44) http://alfawzan.af.org.sa/node/2150
  • Imechapishwa: 06/09/2020