Ni kwa nini leasing ni haramu?

Swali: Ni kwa nini leasing imeharamishwa?

Jibu: Ni kwa sababu kunakusanywa kati ya biashara mbili zinazotofautiana ambapo kila moja ina hukumu yake. Kwa hiyo haijuzu. Isitoshe bidhaa si yenye kutambulika kwa sababu mtu hajui namna ambavo mkataba unavomalizika. Kwa hivyo ni biashara ya kitu kisichotambulika huko katika mustakabali. Aidha ununuzi haupaswi kuahirishwa. Unatakiwa ufanyike katika maeneo hapohapo na kwa kuhudhuria. Ununuzi wa mustakabali kwa maana ya kwamba nitakuuzia pindi bidhaa itafika bandarini au pindi mtu fulani atakapofika au pindi utapofika mwezi fulani. Ni lazima iwe kwa mahudhurio papohapo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (29)
  • Imechapishwa: 11/02/2022