Ni kwa nini asikufurishwe anayepinga sifa na majina yote ya Allaah?

Swali: Je, anakufuru yule ambaye anapinga baadhi ya sifa za Allaah au zote?

Jibu: Hili linahitaji upambanuzi. Anatakiwa kusimamishiwa hoja kwa sababu anaweza kujahili baadhi ya sifa. Anatakiwa kubainishiwa yale yaliyofahamishwa na Qur-aan na Sunnah. Akipinga Mwingi wa huruma (ar-Rahmaan), Mwenye nguvu zisizoshindikana (al-´Aziyz), Mwingi wa hekima (al-Hakiym), Mtakasifu aliyetakasika (al-Qudduus), mfalme (al-Malik) anakufuru. Akiwa ni mtu ambaye si msomi abainishiwe yale yaliyotajwa ndani ya Qur-aan na Hadiyth Swahiyh.

Swali: Vipi ikiwa anapindisha maana ya sifa?

Jibu: Kupindisha maana ya sifa kunatofautiana. Ni kama mfano wa ´Ashaa´irah. Wako ambao wanawakufurisha na wengine hawafanyi hivo. Kupindisha maana ya sifa ni jambo lina shubuha. Ni tofauti na Mu´tazilah na Jahmiyyah ambao ni makafiri. Kwa sababu wamepinga sifa zote na wakapinga pia majina.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-is-Shubuhaat, uk. 100
  • Imechapishwa: 13/08/2019