Ni kitabu kipi bora kinachozungumzia mambo yanayomtoa mtu katika Uislamu?


Swali: Kuna umuhimu kiasi gani ya kujua vikwazo vya Takfiyr? Ni kitabu kipi kizuri katika maudhui haya?

Jibu: Ni lazima kwa mtu kujua mambo yenye kukufurisha. Akishayajua basi ajizuie nayo. Kitabu bora ni hiki cha Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab ambacho hivi sasa tunakisherehesha. Ni kitabu kifupi na chenye kuenea. Vilevile kuna mlango katika vitabu vya Fiqh katika kila madhehebu ambao umetengwa ukibainisha vitenguzi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 33-34
  • Imechapishwa: 11/05/2018