Ni kipi kinachomlazimu mwanamke mwenye nifasi wakati wa kumaliza damu yake ya uzazi?

Swali 176: Ni kipi kinachomlazimu mwanamke mwenye nifasi wakati wa kumaliza damu yake ya uzazi?

Jibu: Ni lazima kwake kuoga kama ambavyo ni lazima vilevile kwa mwanamke mwenye hedhi. Dalili ya hayo ni:

1- Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia: “Wanawake wenye nifasi wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakikaa siku arubaini.

2- Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia: “Mwanamke katika wanawake wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikaa katika nifasi nyusiku arubaini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hamwamrishi kulipa swalah za kipindi cha nifasi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 71
  • Imechapishwa: 06/10/2019