Ni kipi kinachomlazimu mtu ambaye amemwingilia mke wake kwenye tupu ya nyuma?

Swali: Ni kipi kinachomlazimu mtu ambaye amemwingilia mke wake kwenye tupu ya nyuma? Je, kuna mwanachuoni yeyote aliyehalalisha kitendo hicho?

Jibu: Kumwingilia mke kwa nyuma ni kitendo cha haramu kwa mujibu wa Qur-aan, Sunnah na maimamu wote wa waislamu katika Maswahabah, Taabi´uun na wengineo. Allaah amesema katika Kitabu Chake:

نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ وَقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُمْ

”Wake zenu ni konde zenu. Hivyo basi ziendeeni konde zenu vyovyote mpendavyo na tangulizeni kwa ajili ya nafsi zenu.” (02:223)

Imethibiti katika “as-Swahiyh” ya kwamba mayahudi walisema kwamba mtu akimwingilia mke wake kwenye tupu ya mbele kwa kufanya staili kwa nyuma ya basi atazaliwa hali ya kuwa ni mwenye makengeza. Waislamu wakamuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu jambo hilo ndipo Allaah akateremsha Aayah isemayo:

نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ وَقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُمْ

”Wake zenu ni konde zenu. Hivyo basi ziendeeni konde zenu vyovyote mpendavyo na tangulizeni kwa ajili ya nafsi zenu.”

Shamba ni ile sehemu ya maoteo. Mtoto huzaliwa kwenye tupu ya mbele na sio kwenye tupu ya nyuma.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (32/267)