Ni kipi katika ngamia kinachotengua wudhuu´?

Swali: Wudhuu´ unatenguka kwa mwenye kula kitu kingine mbali na nyama ya ngamia kama vile mafuta au ini?

Jibu: Mafuta hapana. Mafuta hayatengui wudhuu´. Maoni sahihi zaidi ni kuwa sehemu nyingine iliyobaki ya ngamia inatengua wudhuu´. Baadhi ya wanachuoni wanasema kuwa vitu vya ndani, ini na [sauti haiko wazi] haviitwi kuwa ni nyama na hivyo havitengui wudhuu´. Haya ndio maoni ya madhehebu. Maoni sahihi ni kuwa vitu vyote vya ngamia vinavyoliwa vinatengua wudhuu´. Kila kitu isipokuwa tu mafuta. Mafuta kwa kukata kabisa sio nyama.

Swali: Mchuzi wa nyama unatengua wudhuu´?

Jibu: Hapana, mchuzi haudhuru. Sio nyama.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (5) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–01041434.mp3
  • Imechapishwa: 27/10/2016