Ni kipi anachohitajia yule anayelingania katika dini ya Allaah?

Swali: Ni elimu ipi ambayo anahitajia mlinganizi anayelingania katika dini ya Allaah na yule anayeamrisha mema na kukataza maovu?

Jibu: Ni lazima kwa mlinganizi anayelingania katika dini ya Allaah na yule anayeamrisha mema na kukataza maovu awe na elimu. Amesema (Ta´ala):

قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي ۖ وَسُبْحَانَ اللَّـهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ

“Sema: “Hii ndio njia yangu: nalingania kwa Allaah, juu ya ujuzi na umaizi – mimi na anayenifuata. Utakasifu ni wa Allaah na mimi si miongoni mwa washirikina.” (12:108)

Elimi ni yale yaliyosemwa na Allaah katika Qur-aan au yaliyosemwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Sunnah Swahiyh. Wote wawili hawa wanatakiwa kutiliwa umuhimu Qur-aan na Sunnah twaharifu ili waweze kutambua yale Allaah aliyoamrisha na yale Allaah aliyokataza. Vilevile atambue mfumo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kulingania kwa Allaah na kukataza maovu na mfumo wa Maswahabah wake (Radhiya Allaahu ´anhum). Ayatambue haya kwa kuvirudilia vitabu vya Hadiyth pamoja na kuitilia umuhimu Qur-aan na kurejelea maoni ya wanachuoni katika mlango huu. Wamelizungumzia hilo kwa upana na wakabainisha yanayotakikana.

Yule anayesimamia jambo hili ni lazima alitilie umuhimu jambo hili ili awe na utambuzi wa Qur-aan na Sunnah na kuyaweka mambo mahala pake stahiki. Matokeo yake ataweka wito katika kheri mahapa pake stahiki na kuamrisha mema katika mahala pake stahiki kwa ujuzi na elimu ili asitumbukie katika lililo baya zaidi kuliko analoenda kukataza au akaenda kuamrisha mema kwa njia ya kwamba kukatokea maovu yaliyo ya khatari zaidi kuliko kuacha ule uovu uliyokuwepo. Ninachotaka kusema ni kwamba ni lazima awe na elimu ili aweze kuyaweka mambo mahapa pake stahiki.

 

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/233)
  • Imechapishwa: 03/07/2017