Swali: Kuna wanaume wanaoomba Zakaat-ul-Fitwr masokoni. Hatujui kama ni watu wa dini au hapana. Kuna wengine hali zao ni nzuri. Ile zakaah wanayopata wanawapa watoto wao. Baadhi yao wanapata mishahara, lakini ni wadhaifu katika dini. Inajuzu kuwapa au hapana?

Jibu: Zakaat-ul-Fitwr wanapewa mafukara waislamu hata kama ni watenda maasi midhali maasi yao hayawatoi katika Uislamu. Kinachotazamwa ni yule mwenye kuipokea hali yake kwa uinje iwe ni ufakiri, hata kama kwa undani atakuwa ni tajiri. Inatakiwa kwa yule anayetoa Zakaat-ul-Fitwr basi ahakikishe kwa kadri ya uwezo wake anaitoa kwa watu wazuri na mafukara. Ikija kuonekana kwamba yule mpokeaji ni tajiri, basi hakuna neno kwa kilichotokea. Bado ni sahihi na himdi zote anastahiki Allaah.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdullaah bin Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alifta.com/Fatawa/FatawaChapters.aspx?View=Page&PageID=58&PageNo=1&BookID=12
  • Imechapishwa: 23/06/2017