Ni kilomita ngapi zinamruhusu mtu kufupisha swalah na kutofunga?

Swali: Ni kilomita ngapi itakuwa ni wajibu kuacha kufunga? Vipi ikiwa mtu atafunga na asile?

Jibu: Baadhi ya wanachuoni wameruhusu kufupisha swalah na kula mchana wa Ramadhaan kwa kile ile ambayo inaitwa “safari”. Wanachuoni wengi wameweka mpaka wa kilomita 80.

Anayefunga kwenye safari ambayo anaruhusiwa kuacha kufunga swawm yake ni sahihi kutokana na dalili zinazofahamisha juu ya hilo. Hakuna neno kwake. Isipokuwa swawm ikimdhuru. Katika hali hii itakuwa imekokotezwa zaidi kwake kula kutokana na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Sio katika wema kufunga safarini.”[1]

[1] Muslim (02/786), Ahmad (03/299), Abu Daawuud (02/796) na wengineo

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/203)
  • Imechapishwa: 06/06/2017