Ni kidole kipi wanamme huvaa pete?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa pete ya fedha?

Jibu: Hakuna neno kuivaa. Ni mamoja katika mkono wa kuume au wa kushoto. Bora ni kuivaa kwenye kidole kidogo, kama  alivovaa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah.

Kuhusu pete ya dhahabu haijuzu kwa wanamme. Dhahabu ni kwa wanawake. Pete ya dhahabu, tai ya dhahabu au vicheni vya dhahabu ni kwa wajili ya wanawake na ni mambo hayatakikani kwa wanamme. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza pete ya dhahabu kwa wanamme. Wakati alipomuona bwana mmoja amevaa pete ya dhahabu akamvua na kuitupa na akasema:

“Atakusudiaje mmoja wenu kuweka kaa la Moto mkononi mwake?”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3975/%D9%85%D8%A7-%D8%A7%D9%84%D8%B3%D9%86%D8%A9-%D9%81%D9%8A-%D9%84%D8%A8%D8%B3-%D8%A7%D9%84%D8%AE%D8%A7%D8%AA%D9%85
  • Imechapishwa: 11/05/2020