Ni katika mfumo wa Salaf kuwajaribu watu kwa watu wengine?

Swali: Je, ni katika mfumo wa Salaf kuwajaribu watu kwa watu wengine?

Jibu: Ndio, ni katika mfumo wa Salaf kumjaribu mtu ambaye kuna mashaka juu yake kutoka kwa watu wa Ahl-us-Sunnah ambaye anamtambua:

”Unasemaje juu ya mtu fulani na fulani?”

Akimzungumza kwa wema na akamsifu kwa undani na kwa uinje, basi mtu huyo sio katika wapotofu wala Ahl-ul-Bid´ah. Lakini akiwasema kwa ubaya au akajibu kiujanja-ujanja na akasema kuwa hamtambui ilihali ukweli wa mambo ni kwamba anamtambua, basi mtu atatambua kuwa si mwenye kufuata mfumo wa Salaf, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Inafaa kuwapa watu mtihani kwa kuwatumia watu wengine wakati kuna haja ya kufanya hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://sahab.net/forums/showthread.php?t=379513
  • Imechapishwa: 28/11/2020