Swali: Kuna mtu ana wake wawili. Mmoja katika wao akamnyonyesha mtoto wa kiume. Je, yule mke mwingine anahitajia kujifunika mbele ya mtoto huyu pindi atapobaleghe?

Jibu: Hapana. Ni mama wake wa kunyonya. Ni kama mfano wa mamake wa kambo. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Unyonyaji unaharamisha yale yanayoharamishwa katika nasabu.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (11) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/14466
  • Imechapishwa: 14/10/2017