Swali: Ni ipi fadhilah ya kufunga siku sita za Shawwaal? Je, ni jambo lenye kuwahusu wanaume na wanawake? Fadhilah zake zinapatikana kwa mtu kufunga mfululizo?

Jibu: Kufunga siku sita za Shawwaal baada ya kumaliza kufunga Ramadhaan ni kama kufunga mwaka mzima. Swawm ni yenye kuenea na inawahusu wanaume na wanawake, ni mamoja mtu akafunga kwa kufululiza au kwa kuachanisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/17)
  • Imechapishwa: 05/06/2019