Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Kipenzi changu wa hali ya juu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliniusia mambo matatu: kufunga siku tatu za kila mwezi, Rak´ah mbili za dhuhaa na niswali Witr kabla ya kulala.”[1]

Wasia wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapomzungumzisha mmoja katika Ummah wake basi ni kwamba amezungumzisha Ummah mzima muda wa kuwa hakuna dalili inayoonyesha kinyume chake.

Kuhusu kufunga siku tatu kila mwezi, ni jambo limepokelewa kwamba ni sawa na kufunga mwaka mzima. Kwa sababu jema moja linalipwa kumi mfano wake na kufunga siku tatu kwa mwezi ni sawa na kufunga mwaka mzima. Shari´ah imejengeka juu ya urahisi na wepesi na fadhilah zinakuwa na uzito mkubwa. Kitendo hichi ni chepesi kwa yule ambaye Allaah amemfanyia wepesi. Hakumtii uzito mtu na wala hakumzuii kufanya shughuli zake akifunga siku hizi. Pamoja na hivyo ndani yake mna fadhilah hizi tukufu. Kwani kila ambavo kitendo ni kitiifu zaidi kwa Mola na ni chenye kumnufaisha zaidi mja, ndivo ambavo kinakuwa pia bora. Aidha kumethibiti mapendekezo ya kufunga siku sita za Shawwaal, siku ya ´Arafah, tarehe 9 na 10 za Muharram na siku ya jumatatu na alkhamisi.

[1] al-Bukhaariy (1178), Muslim (721), at-Tirmidhiy (760), an-Nasaa’iy (1677), Abu Daawuud (1433) na Ahmad (7098, 7140 na 7409).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bahjat-ul-Abraar, uk. 85-86
  • Imechapishwa: 25/02/2021