Swali: Ni ipi tofauti kati ya hali hii[1] na yule aliyepata kujua kuandama kwa mwezi katikati ya mchana?

Jibu: Tofauti iko wazi. Dalili ikisimama katikati ya mchana basi ni wajibu kwao kujizuia. Mwanzoni mwa mchana walikula kutokamana na udhuru wa kutojua. Kwa ajili hii iwapo wangelikuwa wanajua ya kwamba siku hii ni Ramadhaan ingelikuwa ni wajibu kwao kufunga. Kuhusu wale wengine ambao tumewaashiria wanatambua kuwa ni Ramadhaan lakini hata hivyo wameruhusu kutofunga. Kwa hivyo kuna tofauti ya wazi.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/ni-lazima-kwa-anayepata-hedhi-na-nifasi-mchana-wa-ramadhaan-kujizuia/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/104)
  • Imechapishwa: 03/06/2017