Swali: Ni ipi tofauti kati ya Tarawiyh na Qiyaam-ul-Layl?

Jibu: Swalah ya Tarawiyh ndio Qiyaam-ul-Layl. Lakini waislamu wameifanya kuwa mwanzoni mwa usiku kwa sababu ndio sahali zaidi kwa watu kuliko mwishoni mwa usiku. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakusimama usiku mzima isipokuwa katika yale masiku kumi ya mwisho. Masiku hayo ndio alikuwa akisimama usiku mzima. Ama masiku ya mwanzo ya mwezi alikuwa akisimama kuswali na akilala. Pamoja na haya hakusimama kuswali pamoja na Maswahabah zake isipokuwa nyusiku tatu kisha akaacha kwa sababu ya kuchelea isije kufaradhishwa kwa watu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1585
  • Imechapishwa: 13/03/2020