Swali 108: Ni ipi kubwa zaidi Jihaad ya elimu au Jihaad ya silaha?

Jibu: Jihaad ya elimu ni aula zaidi. Ni lazima kwa mtu ajifunze yale yatayomuwezesha kusimamisha dini yake:

فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مُتَقَلَّبَكُمْ وَمَثْوَاكُمْ

“Basi jua kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na omba msamaha kwa dhambi zako na kwa ajili ya waumini wa kiume na waumini wa kike. Allaah anajua harakati zenu huku na kule na pahala penu pa kupumzikia.”[1]

Ameanza kwa elimu kabla ya kuzungumza na kutenda. Elimu ndio yenye kutangulia kisha Jihaad inakuja baadaye ili Jihaad yake hiyo iwe imejengeka juu ya elimu na yakini na isiwe imejengeka juu ya ujinga na makosa.

Swali: Ni wepi ambao wana hadhi za juu zaidi mbele ya Allaah; ni wale wanaopambana na wanafiki au ni wale wanaopambana na makafiri?

Jibu: Wote. Wote wana ujira mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala); wale wanaopambana na wanafiki na wale wanaopambana na makafiri. Wanafiki wanapigwa vita kwa mdomo, kalamu na kufichukua shubuha zao. Huu ni mlango mkubwa kwa sababu ni kuutetea Uislamu na dini. Vivyo hivyo kupambana na makafiri. Lakini – na Allaah ndiye anajua zaidi – kupambana na makafiri ndio jambo kubwa zaidi. Kwa sababu kupambana na makafiri ndani yake kunapatikana manufaa makubwa zaidi. Kwa sababu Mujaahid kunampelekea khatarini na kunampelekea majeraha. Kuhusu kupambana na wanafiki hakumpelekei khatarini na hakumpelekei majeraha mfano wa Mujaahid ambaye anapambana na makafiri. Lakini hata hivo haina shaka kwamba yule anayepambana na wanafiki ana ujira mkubwa.

[1] 47:19

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 301
  • Imechapishwa: 23/11/2019