Ni ipi hukumu ya wanawake kufanya mazoezi?

Swali: Ni ipi hukumu ya msichana kufanya mazoezi?

Jibu: Mazoezi ni neno la jumla na yanatofautiana. Mazoezi kati ya wanawake katika mambo yasiyokwenda kinyume na Shari´ah iliyotakasika kama mfano wa kutembea sana mahali ambapo ni wao wenyewe na hawachanganyikani na wanamme na wala wanamme hawawaoni, kuogelea nyumbani kwao au katika masomo yao ambapo ni wao wenyewe ambapo wanamme hawawaoni na wala hawawasiliani nao ni kitu kisichodhuru.

Kuhusu mazoezi ambapo wanachanganyikana kati ya wanamme na wanawake, wanamme wakawaona au kukasababisha shari kwa waislamu haijuzu. Kwa hivyo ni lazima kupambanua.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/7001/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%85%D8%A7%D8%B1%D8%B3%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%B3%D8%A7%D8%A1-%D9%84%D9%84%D8%B1%D9%8A%D8%A7%D8%B6%D8%A9
  • Imechapishwa: 10/03/2021