Ni ipi hukumu ya waislamu kuleta wafanyakazi makafiri na kuwahudumikia makafiri katika manyumba yao?


Swali: Ni ipi hukumu ya kuleta wafanya kazi ambao ni makafiri na kuwapa chakula?

Jibu: Waislamu ni bora kuliko makafiri. Allaah (Ta´ala) amesema:

 وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ

“Mtumwa muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni.”[1]

Lakini hata hivyo hakuna neno mtu akawaleta wasiokuwa waislamu kwa sababu ya haja.

Kuhusu kuwapa chakula ikiwa ni kwa njia ya huduma ambapo anawahudumikia katika manyumba yao na mfano wa hayo, hapo itakuwa haitakikani. Wanachuoni wametaja machukizo juu ya hilo. Ikiwa sio kwa njia kama hii kama kwa mfano akawapa chakula akiwa nyumbani kwake hakuna neno kwa sababu haja imepelekea kufanya hivo.

[1] 02:221

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (03/41)
  • Imechapishwa: 09/06/2017