Swali: Ni ipi hukumu ya Udhhiyah? Ni ipi hukumu ya kumpwekesa maiti kwa Udhhiyah?

Jibu: Udhhiyah ni Sunnah iliokokotezwa kwa yule mwenye uwezo. Mtu anatakiwa achinje kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya watu wa nyumbani kwake.

Ama kuhusu kuchinja kwa ajili ya maiti sio Sunnah. Kutokana na ninavyojua haikupokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba alichinja Udhhiyah kwa ajili ya maiti yeyote Udhhiyah ya kipekee. Wala jambo hilo halikupokelewa kutoka kwa Maswahabah zake katika uhai wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini mtu anatakiwa kuchinja kwa ajili yake yeye na watu wa nyumbani kwake. Akinuia maiti awe pamoja nao hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (25/10)
  • Imechapishwa: 19/08/2018