Ni ipi hukumu ya swawm ya mwanamke anayetokwa na damu isiyokuwa hedhi wala nifasi?

Swali: Mwanamke ambaye anatokwa na damu ya ugonjwa amehalalika kwa mume wake?

Jibu: Mwanamke mwenye kutokwa na damu hii ni yule anayetokwa na damu ambayo si hedhi wala si damu ya uzazi. Hukumu yake ni kama hukumu ya mwanamke aliye msafi. Hivyo anatakiwa kufunga, kuswali na amehalalika kwa mume wake. Anatakiwa kutawadha juu ya kila swalah. Ni kama mfano wa wale ambao wanakuwa na hadathi yenye kudumu itokamanayo na kutokwatokwa na mkojo na upepo hovyo. Ni wajibu kwake kujihifadhi kutokamana na damu kwa kuweka pamba au kitu kingine ili asijichafue mwili wake au nguo zake.  Hivyo ndivyo zilivyosihi Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/195)
  • Imechapishwa: 20/05/2018