Ni ipi hukumu ya swawm mzazi ambaye damu yake imekauka kabla ya kutimiza masiku arubaini?

Swali: Mwanamke alikuwa na damu ya uzazi na akasafika kabla ya kukamilisha siku arubaini ambapo akaoga na kufunga siku zilizobaki za Ramadhaan baada ya kuona kuwa kweli amesafika. Ameambiwa kwamb ni lazima kulipa zile siku alizofunga kabla ya kutimiza siku arubaini. Ni ipi hukumu ya Shari´ah juu ya hilo? Je, arudi swawm yake au hapana? Je, inajuzu kufanya jimaa baada ya kusafika lakini kabla ya kutimiza siku arubaini au hapana? Je, inajuzu vilevile kufanya jimaa endapo atasafika na hedhi kabla ya kutimiza siku saba?

Jibu: Mambo yakiwa kama alivosema kwamba aliona amesafika kabla ya kutimiza masiku arubaini ambapo akaoga na kufunga, basi funga yake katika yale masiku kabla ya kutimiza siku arubaini ni sahihi na wala halazimiku kulipa. Hapana vibaya kufanya jimaa katika kipindi cha yale masiku – yaani yale masiku ambayo alisafika na akaoga kabla ya kutimiza masiku arubaini – kama ambavyo pia hapana vibaya kufanya jimaa baada ya kusafika kutokamana na hedhi kabla ya kutimiza siku saba.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/197-198)
  • Imechapishwa: 20/05/2018