Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya kupatwa kwa jua?

Jibu: Ni Sunnah iliyokokotezwa. Kuna wanachuoni wengine wanaonelea kuwa ni faradhi kwa baadhi ya watu. Pindi wanachuoni wanapotaja swalah zilizopendekezwa wanasema kuwa iliyokokotezwa zaidi ni swalah ya kupatwa kwa jua, kisha swalah ya kuomba mvua halafu Tarawiyh. Kwa hivyo ni Sunnah iliyokokotezwa kwa mujibu wa madhehebu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (58) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/16539
  • Imechapishwa: 23/09/2017