Ni ipi hukumu ya Shari´ah kwa ambaye limekariri kwake jambo la kuuza dawa za kulevya?

Swali: Ni ipi hukumu ya Shari´ah kwa ambaye limekariri kwake jambo la kuuza dawa za kulevya?

Jibu: Kilicho cha lazima ni kumsimamishia adhabu ya ki-Shari´ah. Likikariri kwake jambo hilo asimamishiwe adhabu. Hapana vibaya kumuaziri kwa kumfunga jela na mengineyo ambayo yatamzuia kuyatumia. Baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa auliwe ikiwa kumtia adabu, kumuaziri na adhabu za ki-Shari´ah hazikumfaa. Hicho ni kiungo kilichooza ambacho kinapaswa kuuliwa kisije kuharibu jamii na ummah. Anatakiwa kusimamishiwa adhabu mara kwa mara mpaka Allaah amwongoze au afe.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4418/ما-حكم-من-تكرر-منه-تعاطي-المخدرات
  • Imechapishwa: 17/06/2022