Ni ipi hukumu ya mwanamke kuacha uso wake wazi?

Swali 1040: Ni ipi hukumu ya mwanamke kuacha uso wake wazi na kutoka kwake mbele za wanaume ambao ni kando na yeye?

Jibu: Ni jambo lenye kutambulika fika kwamba kitendo cha waislamu, wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wakeze Maswahabah katika zama zake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), zama za makhaliyfah waongofu na wema waliotangulia kwamba haifai kwa mwanamke kutoka akiwa uso wazi. Maandiko ya Kishari´ah kutoka katika Qur-aan, maneno ya Salaf wa Ummah na wale waliokuja baada yao ni mengi na yenye kutambulika. Aidha Allaah amewaamrisha jambo hilo wakeze waumini. Amesema (Ta´ala):

وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ

“…  wajiteremshie jilbaab zao.”[1]

Ibn ´Abbaas na wengineo wamefasiri kwamba ni mwanamke kufunika uso wake mbele ya wanaume wa kando.

Upande wa kuacha Hijaab haukuwekwa isipokuwa kwa wale wanawake watuwazima kwa sharti ya kutojishauwa kwa kuonyesha mapambo. Amesema (Ta´ala):

وَالْقَوَاعِدُ مِنَ النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا يَرْجُونَ نِكَاحًا فَلَيْسَ عَلَيْهِنَّ جُنَاحٌ أَن يَضَعْنَ ثِيَابَهُنَّ غَيْرَ مُتَبَرِّجَاتٍ بِزِينَةٍ

“Wanawake wazee waliokatika hedhi wasiotarajiwa kuolewa, hakuna neno juu yao kupunguza baadhi ya nguo zao pasi na kudhihirisha mapambo yao.”[2]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwanamke ni ´Awrah.”

´Awrah ni lazima ifunikwe yote na wala haijuzu kufunua chochote katika ´Awrah.

[1] 33:59

[2] 24:60

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 423
  • Imechapishwa: 26/03/2020