Swali: Je, inajuzu kwangu mimi kama muislamu kufungua na kusoma Injiyl kwa lengo la kusoma peke yake na si kwa lengo lingine? Je, imani kuhusu kuamini vitabu vya mbinguni inahusiana na kuamini ya kwamba ni vyenye kutoka kwa Allaah au ni sisi kuamini yale yaliyotajwa ndani yake? Tunaomba utupe faida Allaah akujaze kheri.

Jibu: Ni wajibu kwa kila muislamu kuamini ya kwamba ni vyenye kutoka kwa Allaah. Inahusiana na Tawraat na Injiyl. Tunatakiwa kuamini kwamba Allaah kateremsha vitabu kwa Mitume Wake na amewateremshia vilevile maandiko ambayo ndani yake kuna maamrisho na makatazo, mawaidha na makumbusho, maelezo kuhusu baadhi ya mambo yaliyotangulia, kuhusu mambo ya Peponi na ya Motoni na mengineyo. Lakini hata hivyo haifai kwake akaitumia. Kwa sababu ndani yake kumeingia upotoshaji, mabadilisho na mageuzo. Haifai kwake akahifadhi Tawraat, Injiyl au az-Zabuur au akasoma ndani yake. Ndani yake kuna khatari. Huenda akakadhibisha haki au akasadikiha batili. Kwa sababu vitabu hivi vimepotoshwa na kugeuzwa na mayahudi na  manaswara wamevitia mkono ambapo wakavigeuza, wakavibadilisha, kuvipotosha, kuyatanguliza na kuyachelewesha baadhi ya maandiko. Allaah ametutosheleza kwa Kitabu kitukufu; Qur-aan tukufu…

Mimi nakunasihi wewe kama ambavyo nawanasihi wengine pia wasichukue chochote kutoka humo. Ni mamoja kutoka katika Tawraat wala Injiyl. Haifai hata kusoma chochote kutoka humo. Bali mkipata chochote kifukieni au kichomeni moto. Kwa sababu haki iliyomo ndani kumekuja chenye kufanya kutoihitajia; nayo ni Qur-aan. Yaliyoingia ndani yake katika mageuzo na mabadiliko ni uovu na batili. Hivyo ni wajibu kwa muumini kujichunga kutokamana na hilo na atahadhari kusoma ndani yake. Kwa sababu khatari yake huenda akasadikisha batili au akakadhibisha haki. Njia ya usalama ni ima kuvizika au kuvichoma moto.

Ni jambo linaloweza kuwa lenye kufaa kwa mtu ambaye ni msomi kuvisoma kwa ajili ya kuwajibu maadui wa Uislamu katika mayahudi na manaswara. Kama ambavyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alilingania kwa Tawraat baada ya mayahudi kupinga mzinifu ambaye kishaingia katika ndoa kupigwa mawe ambapo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaonyesha. Baada ya hapo wakalikubali. Tunachokusudia kusema ni kwamba wale wanazuoni ambao wanaijua Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) huenda wakahitajia kufunua Tawraat, Injiyl au az-Zabuur kwa malengo ya Kiislamu. Kwa mfano kuwajibu maadui wa Allaah, wakabainisha ubora wa Qur-aan na ile haki na uongofu uliyomo ndani yake. Kuhusu wale wasiokuwa wasomi haifai kwao kufanya hivo. Bali pale watapopata kitu katika Tawraat, Injiiyl au az-Zabuur basi

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/old/38153
  • Imechapishwa: 22/11/2018