Ni ipi hukumu ya mtu mwenye kujiua?

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu ambaye anapigana bega kwa bega akiwa pamoja na waislamu kisha baadaye akajiua nafsi yake? Ni vipi hukumu ya mtu mwenye kujiua kwa kujilipua? Je, atadumishwa Motoni milele au akatolewa ndani yake kwa sababu alikuwa ni mpwekeshaji?

Jibu: Mtu mwenye kujiua nafsi yake au akawaua wengine kwa makusudi basi juu yake ana matishio makali kama ilivyokuja katika Hadiyth:

“Mwenye kujiua nafsi yake ataadhibiwa siku ya Qiyaamah. Mwenye kujiua nafsi yake kwa kisu atakuwa Motoni akijipasua tumbo lake. Mwenye kujiua nafsi yake kwa sumu basi ataila sumu hiyo ndani ya Moto. Mwenye kujiua nafsi yake kwa kujirusha kutoka kwenye mlima au kitu kingine basi atajirusha Motoni.”

Kwa mujibu wa wanachuoni haya ni matishio. Akiwa ni mwenye kuhalalisha kujiua anakufuru. Lakini midhali haonelei kuwa ni halali ni dhambi kubwa tu. Ana hukumu moja kama wale watenda madhambi makubwa. Hatoki katika Uislamu. Lakini juu yake ana matishio makali.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (06) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/433/433.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2018