Ni ipi hukumu ya msafiri kufunga safarini?


Swali: Ni ipi hukumu ya Shari´ah funga ya msafiri?

Jibu: Hukumu ya msafiri ni kwamba analo chaguo; akitaka kufunga basi atafunga, na akitaka kula basi atakula. Ingawa kuacha kufunga ndio bora zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Si katika wema kufunga safarini.”

Akiacha kufunga ndio bora zaidi. Akifunga kwa sababu kufunga ndio kwepesi zaidi kwake hakuna neno. Mara Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake walifunga na mara nyingine wakaacha kufunga.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4423/%D9%85%D8%A7-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D9%81%D8%B6%D9%84-%D9%84%D9%84%D9%85%D8%B3%D8%A7%D9%81%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%88%D9%85-%D8%A7%D9%85-%D8%A7%D9%84%D9%81%D8%B7%D8%B1
  • Imechapishwa: 13/09/2020